Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2018
Picha
 MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KILIMANJARO IVAN MOSHI, NNE KULIA AKIFUATIWA NA KATIBU WA UVCCM MKOA WA KILIMANJARO, ABDULRAHIM HAMAD, WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WAJUMBE WA BARAZA KUU LA VIJANA WILAYA YA SIHA JUZI.  MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (UVCCM), MKOA WA KILIMANJARO IVAN MOSHI (aliyesimama), AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA BARAZA LA UMOJA HUO WILAYA YA HAI JANA. KATIBU WA UMOJA WA VIJANA MKOA WA KILIMANJARO, ABDULRAHIM HAMAD AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA BARAZA LA UVCCM WILAYA YA SIHA JUZI.

MWENYEKITI WA UVCCM ATANGAZA KIAMA KWA WANAOCHEZEA MAENDELEO YA VIJANA.

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro (UVCCM), Ivan Moshi ametangaza kiama kwa watumishi wa Serikali katika mkoa huo watakaokiuka matakwa ya Serikali ya kutenga fedha za vijana ambazo ni asilimia nne (4), ya makusanyo ya mapato ya  ndani ya Halmashauri. Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo jana katika Baraza la vijana la wilaya ya Hai ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika wilaya zote za mkoa huo lengo likiwa ni kuhamasisha mabaraza ya umoja wa vijana wilaya kugeuka kuwa vikundi vya maendeleo (Community Based Organization). Moshi alisema kuwa, serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kuwanufaisha vijana lakini fedha hizo zimekuwa zikishindwa kuwanufaisha kutokana na vijana kutopatiwa elimu ya kutosha juu ya uanzishwaji wa vikundi pamoja na kuandika maandiko ya miradi. "Katika ziara yangu niliyoianza Same, Mwanga, Siha na leo nipo hapa Hai nimegundua kuwa vijana wengi hawana elimu ya uanzishaji wa vikundi pamoja na na kushindwa kuandika m...