MWENYEKITI WA UVCCM ATANGAZA KIAMA KWA WANAOCHEZEA MAENDELEO YA VIJANA.
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro (UVCCM), Ivan Moshi ametangaza kiama kwa watumishi wa Serikali katika mkoa huo watakaokiuka matakwa ya Serikali ya kutenga fedha za vijana ambazo ni asilimia nne (4), ya makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo jana katika Baraza la vijana la wilaya ya Hai ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika wilaya zote za mkoa huo lengo likiwa ni kuhamasisha mabaraza ya umoja wa vijana wilaya kugeuka kuwa vikundi vya maendeleo (Community Based Organization).
Moshi alisema kuwa, serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kuwanufaisha vijana lakini fedha hizo zimekuwa zikishindwa kuwanufaisha kutokana na vijana kutopatiwa elimu ya kutosha juu ya uanzishwaji wa vikundi pamoja na kuandika maandiko ya miradi.
"Katika ziara yangu niliyoianza Same, Mwanga, Siha na leo nipo hapa Hai nimegundua kuwa vijana wengi hawana elimu ya uanzishaji wa vikundi pamoja na na kushindwa kuandika maandiko ya miradi hali ambayo imekuwa ikiwasababishia kushindwa kunufaika na fedha zinazotengwa na Halmashauri" alisema Moshi.
Alisema kuwa, wapo baadhi ya watendaji wa Halmashauri ambao sio waaminifu wamekuwa wakitenga fedha hizo kidogo tofauti na matakwa ya kisheria huku pia baadhi ya madiwani wamekuwa wakiunda vikundi vyao na kwenda kuzitafuna fedha hizoa ambapo alitanga kiama kwa viongozi wanaotenda vitendo hivyo.
"Katika uongozi wangu huu sitakubali kuona maslahi ya vijana yakichezewa na watu wachache nitapambana na yeyote atakayekuwa mstari wa mbele kurudisha nyuma maendeleo ya vijana bila kujali cheo chake maana nimepewa dhamana ya kuwatumikia vijana na kuona wanasonga mbele kimaendeleo" alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa, wapo baadhi ya Viongozi wa chama wamekuwa wakiwatumia vijana kwa maslahi yao binafsi na kuahidi katika uongozi wake hatakubali kuona vijana wakitumika kwa ajili ya maslahi ya viongozi wengine.
Moshi alisema kuwa, Umoja wa vijana umekuwa ukikosa fedha za kuendeshea shughuli za kiofisi hali ambayo imekuwa ikiwalazimu kuomba misaada kwa watu mbalimbali na kudai kuwa kugeuzwa kwa mabaraza ya wilaya kuwa vikundi vya maendeleo vitaondoa changamoto ya kuomba fedha kwa watu na badala yake itasaidia kujiendesha yenyewe.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza kuu la Vijana Taifa, kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Nice Munisi alisema kuwa, kwa sasa wamejipanga kuhakikisha kuwa vijana wanatambua vyanzo vya mapato vilivyopo pamoja na kutambua mbinu mbalimbali za kujiinua kiuchumi zilizopo ili kuwaondoa katika mfumo wa kulalamika.
Munisi alisema kuwa, fura nyingi zipo Serikali isipokuwa vijana wengi wamekuwa hawatambua fursa hizo hivyo wameanza kuwahamasisha vijana kujiunga katika vikundi ili kuweza kukopa fedha halmashauri na kuzitumia katika kujiletea maendeleo.

Maoni
Chapisha Maoni